Ingawa inaonekana kuwa hatari, daoliao, ambayo hutafsiriwa kama “masaji ya kisu” au “tiba ya kisu”, inaaminika kuwa na nguvu za uponyaji wa mwili na kihemko na ni aina ya dawa ya Wachina ambayo inadhaniwa kuwa na zaidi ya miaka 2,000.
Wataalamu wanasema ilifanywa kwanza na watawa katika China ya zamani. Ilienea hadi Japan katika Enzi ya Tang zaidi ya miaka 1,000 iliyopita na kwa Taiwan kufuatia Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China miaka ya 1940.
Kukanda kwa kwa namna hiyo ni ngumu kuona leo nchini China na Japan, imeibuka tena nchini Taiwan katika miaka ya hivi karibuni kwani watu wameitafuta kutibu mifadhaiko ya maisha ya kisasa.
Kituo cha elimu ya sanaa ya kale ya kuchua kwa kisu Dao Liao I-Jing huko Taipei kimewafundisha watendaji kwa karibu miongo minne. Wana matawi 36 huko Taiwan, 15 ambayo yamefunguliwa katika miaka mitano iliyopita. Wamefundisha pia watu kutoka ulimwenguni kote, kutoka Japan hadi Hong Kong, Ufaransa hadi Canada.
Leo, watu hutafuta visu vya wataalam kusaidia kupunguza magonjwa ya mwili, kuboresha hali ya usingizi na kukabiliana na uchungu wa kuachwa.
Wataalamu wana sheria fulani za kufuata. Kwa mfano, ikiwa wako na mhemko mbaya, hawapaswi kuwakanda watu kwa kutumia kisu “watahamishia hasira mbaya kwa mteja,” kulingana na Hsiao ambae ni mtaalam wa masaji. Kwa hali yoyote, kutumia visu wakati wa hali hiyo sio jambo zuri.
Ili kujiweka sawa , watendaji wote hula vyakula vitokanavyo na mbogamboga, matunda na karanga . Hsiao na jeshi lake la wataalam pia huamka mapema kila asubuhi na kufanya mazoezi ya viungo na pia kwa kutumia visu kwa dakika 30.
Ni kazi nyingi kwa wataalamu – lakini pia kwa wateja. Kabla ya kukandwa mteja huambiwa afanye mazoezi ya kuchuchumaa kwa dakika 10 akiwa pamoja na mtaalam wa masaji na hushikilia “vijiti” vya mbao mikononi mwao.
Hsiao anasema wazazi hupeleka watoto kucheza na vijiti kupunguza misongo ya mawazo inayotokana na shule.
Hsiao alisema hakuhitaji kumshawishi mtu yeyote juu ya ufanisi wa tiba ya kisu, kwani watu wataamini hata hivyo ikiwa utawatibu magonjwa yao. “Watakwenda kwenye maduka mengi au [kujaribu] tiba tofauti … na baada ya [uzoefu] wao watapata bora zaidi,” alisema.
Wateja walisema kuchua kwa kisu ilikuwa uzoefu badala ya kuchua kawaida tu. waliondoka wakitafakari . Lakini bila shaka walikuwa wamepumzika. hulala mapema, na hulala hadi asubuhi iliyofuata wakati bila shaka, na kisha nikalala kwa saa kadhaa nyingine.
Namna “masaji” hiyo inavyofanyika kwa mujibu wa mteja
Nikiwa nimelala uso ukiwa umeegemea meza maalumu ya kukanda, nilisubiri kwa hofu. Mtaalamu wa kuchua kwa kutumia kisu, Elsa, kwa bashasha alikuwa ameshika visu viwili. Hii ni kwasababu wakati mwendo wa kukata unatarajiwa katika kuukanda mwili, katika hii, visu hufanya mithili ya ukataji.
Elsa alianza kwa kutumia mikono yake kuukanda mwili wangu. Kisha visu baridi, vya chuma vilianza kupita, juu ya mgongo wangu, mikono na kichwa changu. Nisingejua kuwa visu vilikuwa kazini kama haikuwa sauti ya visu vilivyokuwa vinagongana mara kwa mara.
Wakati kukata kulimalizika, lazima ningekuwa nimelala. cha kushangaza, watu wengi husinzia wanakandwa na visu kwa dakika 70