Watanzania wanayo nafasi ya kupata ajira ya Ualimu kwenye nchi mbalimbali Duniani, ambazo zimeingiza somo la Kiswahili katika mitaala yao.
Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Kiswahili duniani katika ukumbi wa Chuo cha Polisi, Ziwani Zanzibar.
Amesema, “Watanzania tunayonafasi ya kufundisha Kiswahili nje ya nchi, tuitumie vizuri fursa hii, tuamke na tuone nafasi yetu kwenye kuzitumia fursa hizi.”
Aidha, Waziri Mkuu pia ametoa wito kwa Watanzania kuzungumza na kusoma lugha ya Kiswahili kiufasaha kwani kuwa mzawa wa lugha pekee, haitawezesha kunufaika na fursa husika.