Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema Kiswahili kimekubalika kuwa moja ya Lugha ya Mawasiliano zitakazotumika katika Umoja wa nchi zinazozalisha madini ya Almasi Afrika (African Diamond Producers Association) ADPA.

Waziri Biteko amesema hayo wakati akifunga Mkutano wa 7 wa Mawaziri wa nchi za umoja huo, uliofanyika kwa njia ya Video ambapo amesema kuwa Kiswahili kinaongezeka kwenye lugha zilizokuwa zinatumika awali ambazo ni Kiingereza, Kireno na Kifaransa.

Mkutano huo wa 7 wa Mawaziri wa Nchi zinazozalisha madini ya Almasi Afrika, umehudhuriwa na nchi zote 19 wanachama wa umoja huo.

Baadhi ya Nchi hizo ni Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini, Namibia, Tanzania, Zimbabwe, Cameroon, Afrika ya Kati, Ghana, Togo, Guinea na Sierra Leone, Algeria, Jamhuri ya Congo, Cote D’ivore, Gabon, Liberia, Mali na Mauritania.

Ajira mpya 6000 zawasubiri walimu
Mume wa Malkia Elizabeth, Prince Philip afariki