Muungano wa Afrika (African Union) umeipitisha lugha ya Kiswahili, kuwa lugha rasmi ya kikazi ndani ya Umoja huo. Lugha hiyo huzungumzwa katika nchi kadhaa za Mashariki mwa Afrika pamoja na jamii za Waswahili katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu na Oman.
Huu ni uamuzi ambao umekuwa ukitarajiwa kwa miongo kadhaa sasa. Miaka mingi watu wamekuwa wakiuliza kwa nini ni lugha moja tu ya nchi za Kiafrika iliyo lugha rasmi ya Muungano wa Afrika (African Union)?
Akizungumza katika kipindi Cha mahojiano Cha Dar24Media Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na Mwalimu Mstaafu wa kiswahili Said Miraji amesema kutumika kisawahili katika mikutano ya AU ni kama kufungua mipaka kwa lugha hiyo, huku akielezea faida ya lugha hiyo kutumika ni pamoja na kukuza mahusiano ya kimaendeleo.
Aidha Mchambuzi Miraji amesema ni wakati sasa wa Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA na Baraza la Kiswahili Zanzibar BAKIZA kutengeneza misamiati ya kutosha Ili kuepusha changamoto ya kiswahili kukosa misamiati.
Amesema ni wakati sasa kama nchi kuandaa Walimu zaidi wa lugha ya kiswahili Ili kutumika fursa ya kufundisha kiswahili kwa nchi za kimataifa.