Kitambulisho cha rais wa Urusi, Vladimir Putin alichopewa kama jasusi nchini Ujerumani alipokuwa anafanya kazi kama jasusi wa Urusi kimepatikana katika makavazi jijini Dresden.
Rais huyo wa Urusi amekuwa mara kwa mara akisema anajivunia kazi aliyoifanya akiwa kama jasusi wa idara ya ujasusi ya Urusi wakati huo ikifahamika kama KGB jijini Dresden miaka ya 1980, ambapo KGB kwa kirefu ni Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti (Kamati/Idara ya Usalama wa Taifa).
Aidha, Putin wakati huo alipewa kitambulisho hicho na idara ya ujasusi ya Ujerumani Mashariki ambayo wakati huo ilikuwa chini ya Muungano wa Usovieti (USSR).
Idara ya ujasusi ya Ujerumani Mashariki ilifahamika kama Stasi, lakini kwa kirefu ni Ministerium für Staatsicherheit kwa maana ya maajenti wa Idara ya Usalama wa Taifa.
-
Rais wa zamani apigwa marufuku kukanyaga Marekani
-
Waziri kuitwa ‘Kahaba’, Afrika Kusini yaiwakia Rwanda
-
Video: Ndege za kivita za Urusi zaichefua Marekani
Hata hivyo, kitambulisho cha Stasi alichokitumia Putin kimegunduliwa wakati wa uchunguzi kuhusu ushirikiano wa karibu uliokuwepo kati ya KGB na Stasi.