Kikosi cha Kitayosce FC (Tabora United) kimeanza kuingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na Msimu ujao wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi ujao.

Kitayosce FC (Tabora United) itashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza, ikitokea Championship, ambako ilimaliza katika nafasi ya pili, nyuma ya Mabingwa wa Ligi hiyo JKT Tanzania.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya wachezaji walioipandisha timu hiyo wametemwa na waliosalia wapo nane pekee, ambao wataungana na wanaoendelea kusajiliwa katika kipindi hiki.

Mmoja wa viongozi amesema wamefikia hatua ya kuacha wachezaji wengi walioipandisha timu kutokana na ugumu wa mashindano yaliyopo mbele yao.

Tunataka kuwa na timu nzuri kwa ajili ya kutimiza malengo ya msimu, nadhani kila kitu kitakuwa sawa tuanza maandalizi ya msimu.”

“Tumeshuhudia mara kadhaa timu zikipanda daraja lakini hazidumu hivyo uongozi umeamua kufanya mabadiliko hayo ili kuendana na kasi ya ligi tutakayoshiriki.

“Wachezaji wameanza kuwasili tangu jana Jumatatu (Julai 10) na kesho Jumatano (Julai 12) wataanza mazoezi mepesi hivyo hadi juma hili likimalizika tayari wachezaji wote watakuwa wamewasili hata wale wa kutoka nje ya nchi,” amesema mtoa taarifa huyo.

Moja ya wachezaji waliosalia ni mfungaji bora wa timu hiyo, Fabrice Ngoy aliyemaliza msimu na mabao 15 nyuma ya Edward Songo wa JKT Tanzania aliyekuwa kinara kwa mabao 18.

Hata hivyo, taaarifa za ndani zinaeleza tayari wamemalizana na Mlinda Lango kutoka Cameroon, beki kutoka Al Hilal na Asec Mimosas, ambao wanatarajia kutua nchini kesho Jumatano (Julai 12).

Benchi la Ufundi la Kitayosce FC (Tabora United) kwa sasa linaongozwa na Kocha Henry Nkamwa, wakati Kocha Mkuu akitazamiwa kutangazwa juma lijalo baaada ya mabosi kupitisha jina moja kati ya wale waliopendekezwa.

Nkamwa amesema ripoti ya benchi la ufundi baada ya kumalizika kwa Ligi ya Championship ilikuwa kuongeza nguvu zaidi eneo la Mlinda Lango na Beki.

“Kuhusu nani ameshasajiliwa kati ya wale tuliopendekeza bado sijajua, nitakupa jibu,” amesema Kocha Nkamwa.

Postecoglou kumuweka chini Harry Kane
Mganga Mfawidhi asimamishwa kazi, Waziri apongeza