Taarifa zilizokuwa zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na magazetini kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa ataibuka kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM leo, zimejibiwa na mwanasiasa huyo.

Mtu wa karibu wa mwanasiasa huyo amesema kuwa ameongea naye na amekanusha taarifa hizo na kueleza kuwa hana mpango wa kushiriki katika kampeni za mwaka huu kukipigia debe chama chochote.

“Dk. Ameupuuza uvumi huo kwa sababu hauna ukweli wowote pia amesema hatajihusisha na kampeni za Ukawa wala CCM. Kwa sasa anasema amejisikia huru kukaa mbali na siasa na hafikirii hata kidogo kujihusisha na siasa labda baada ya uchaguzi mkuu,” aliliambia gazeti la Mtanzania.

Dk. Slaa alijiweka kando na siasa tangu Chadema ilipomkaribisha Edward Lowassa katika chama hicho na kumpa nafasi ya kugombea urais akiwakilisha Ukawa.

Leo, Chama Cha Mapinduzi kitazindua kampeni zake za kumnadi mgombea urais, Dk. John Magufuli katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.

CCM Kugawa Mamilioni Kila Kijiji
Kilichomkera Zaidi Sumaye CCM, Alijeruhiwa Muda Mrefu