Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa anaridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa DAWASCO katika kusimamia miradi mbalimbali ya maji.
Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji inayosimamiwa na DAWASCO, amesema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kutoa huduma za maji kwa wakazi zaidi ya laki mbili wa mikoa ya Pwani na Dar es salaam.
“Kwa ujumla naridhishwa na kazi inayofanywa na DAWASA katika kutekeleza miradi ya maji nawatia moyo muendelee kufanya kazi hii kwa bidii ili azma ya Serikali kuwafikishia wananchi huduma ya maji kwa wakati itimie,”amesema Mkumbo.
Hata hivyo, Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na umwagiliaji kukagua miradi inayotekelezwa na DAWASA katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani imehusisha vyanzo vya maji vya Ruvu Juu, Mradi wa uchimbaji Visima virefu Kimbiji na Mpera, Chanzo cha maji Wami unakotekelezwa mradi mkubwa wa upanuzi na ulazaji mabomba, ujenzi wa vituo vya kusambazia maji na matanki ya kuhifadhi maji Chalinze.