Serikali mpya ya Rais John Magufuli inaonekana haijajua namna ya ‘kudeal’ na upinzani, na upinzani nao unaonekana haujajua namna ya ‘kudeal’ na serikali mpya.

“Bado tunaendesha siasa zetu za upinzani kama tulivyofanya wakati wa JK, ambaye ‘style’ yake ya uongozi ilikuwa tofauti mno na huyu Rais wa sasa. Lazima kujipanga upya. Tunahitaji kukaa chini na kuchora ramani mpya ya namna ya kuendesha siasa za upinzani katika kipindi hiki. Kimsingi upinzani Tanzania ulitarajiwa kupanda ngazi kwa mwendo wa konokono (evolutionarily) lakini kuna uwezekano mkubwa katika kipindi hikin ukapanda ngazi kwa kasi ya kimapinduzi (revolutionarily).

“Hata hivyo ni lazima kujipanga upya-hili halitawezekana kwa kufanya siasa za aina ile ile na kwa mtindo ule ule.”

 

Young Dee akiri kutumia dawa za kulevya, aomba radhi
Al-Shabab lakiri kumuua afisa wa usalama Somalia