Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limethbitisha kupokea malalamiko ya kimaadili dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora (TAREFA), Yusuph Kitumbo na Kocha Ulimboka Mwakingwe.
TFF imetoa taarifa za kupokea malalamiko hayo kupitia vyanzo vyake vya habari na kukiri kuyafikisha mbele Kamati ya Maadili ya Shirikisho hilo ili yafanyiwe kazi kwa mujibu wa Kanuni za Maadili za TFF, Toleo la 2013.
Taarifa ya TFF imeeleza: Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea malalamiko ya kimaadili dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora (TAREFA), Yusuph Kitumbo na Kocha Ulimboka Mwakingwe.
Malalamiko hayo yanayohusisha madai ya upangaji matokeo yamewasilishwa na klabu ya Ligi ya Championship, Fountain Gate FC.
Tayari malalamiko hayo yamewasilishwa katika Kamati ya Maadili ya TFF ili yafanyiwe kazi kwa mujibu wa Kanuni za Maadili za TFF, Toleo la 2013.
Ili kulinda hadhi ya mpira wa miguu, TFF inawakumbusha wanafamilia wote wa mpira wa miguu kuwa itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na upangaji matokeo.