Kitunguu maji ni aina ya mboga yenye harufu kali inayochangamsha mwili, Pia kitunguu ni kiungo ambacho kina virutubisho katika vyakula na kuvifanya viwe na ladha nzuri.

Imebainika kuwa kitunguu maji kimekuwa kikitibu na kuponya maradhi mbalimbali kutokana na kuwa na salfa ambayo ni nzuri, hasa kwenye ini na husaidia kuponya kansa kwenye utumbo na kinywa kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya vitamini C.

Faida za kitunguu maji katika mwili wa binaadamu ni pamoja na kuupa mwili nishati, kuongeza nguvu, huimarisha misuli ya mwili, huongeza hamu ya kula, hulainisha tumbo na kuondoa tatizo la kukosa choo.

Kinaweza kutibu magonjwa mbalimbali, ikiwemo kikohozi, vidonda vya tumbo na mifupa, figo, tumbo na mkojo, kufunga hamu ya kula.

Licha ya kuwa na umuhimu huo, pia huimarisha afya ya moyo, kuzuia kansa, huukinga mwili dhidi ya vidonda vya tumbo, huongeza joto mwilini na huzuia vimelea vya magonjwa mbalimbali katika mwili wa binaadamu.

Kitunguu maji kinaweza kutengenezewa juisi kwa kukikatakata kisha kukisaga kwa blenda kwa kuchanganya na maji ya kunywa mara unapojisikia vibaya hasa kwa watu ambao wanasumbuliwa na kifua mara kwa mara.

Pia unaweza kuchanganya na asali na kunywa nayo inasaidia kwa kiasi kikubwa kutibu maumivu ya tumbo na uvimbe mwilini. Maji ya kitunguu kwa mujibu wa wataalamu wa tiba wanasema yanatibu matatizo ya macho.

Nchi mashuhuri na maarufu inayolima ni Misri na kusambaa zaidi duniani, kwa hapa Tanzania kinalimwa zaidi katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Arusha na mikoa mingine ambayo ina rutba nzuri ya kustawisha.

Usiyoyajua juu ya maisha ya Mende 'Anaweza kuishi bila kichwa'
Mzee Akilimali atamani kuandamana hadi kwa Waziri mkuu