Serikali ya kijeshi nchini Burkina Faso imesitisha shughuli za moja ya Radio maarufu nchini humo, kutokana na Redio hiyo kudaiwa kufanya mahojiano yanayodharau viongozi wapya wa Kijeshi katika nchi jirani ya Niger.

Tarifa iliyotolewa na Waziri wa Mawasiliano nchini Burkina Faso, Rimtalba Jean Emmanuel Ouedraogo imeeleza kuwa Radio hiyo iitwayo Omega, imezuiwa mara moja kuendelea na shughuli zake kwa kipindi cha muda usiojulikana.

Amesema, hatua hiyo imechukuliwa kutokana na sababu za masilahi ya juu ya nchi huku akidai kituo hicho cha Radio kinamilikiwa na Mwanahabari wa zamani na Waziri wa Mambo ya Kigeniwa Burkinafaso, Alpha Barry.

Katika mahojiano hayo, Kituo hicho kilikuwa kikifanya mahojiano na Msemaji wa Kundi jipya nchini Niger, Ousmane Abdoul Moumouni, linalotaka kurejeshwa madarakani kwa rais Mohamed Bazoum.

Wan-Bissaka afunguka mazito Man Utd
Hofu yatanda uwanja wa Mkwakwani