Kituo cha uwekezaji nchini TIC kimetoa elimu kwa wajasiliamali na kuwataka kujiamini katika shughuli na biashara mbalimbali wanazofanya.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uwekezaji TIC, John Mnali alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kuwa mafunzo hayo ni fursa kubwa kwa wajasiliamali hao kuweza kujikwamua na kujenga uhusiano mkubwa utakao wawezesha kubadilishana uzoefu kati ya wajasiliamali wadogo na wakubwa jinsi ya kukabiliana na changamoto.
“Jukumu la Kituo cha Uwekezaji hapa nchini ni kuhakikisha kuwa wajasiriamali wadogo na wakati wanazalisha bidhaa zitakazotumiwa na makampuni makubwa ya wawekezaji,”amesema Mnali
Hata hivyo, Mnali ameongeza kuwa ili kuhakikisha wajasiliamali wanakuza mitaji yao, Kituo cha Uwekezaji TIC kimeshirikisha taasisi za kifedha katika semina hiyo.