Mahakama nchini Kenya imeamuru kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu katika Kaunti ya Machakos kifungwe mara moja, kufuatia tuhuma kuwa wavulana tisa walikuwa wakinajisiwa kwenye kituo hicho.
Idara inayoshughulikia watoto katika Kaunti hiyo ilipokea amri ya mahakama na kuifanyia kazi jana (Jumatano) ikisaidiwa na jeshi la polisi kufunga kituo hicho kilicho chini ya Kanisa Katoliki.
Wavulana hao tisa wanaodaiwa kuingiliwa na mpishi wa shule hiyo wamepelekwa katika kituo maalum na salama zaidi katika Kaunti hiyo kiitwacho Machakos Rescure Centre and Remand Home.
Kituo hicho cha watoto waishio kwenye mazingira magumu ambacho kina shule ya msingi, kinatunza jumla ya wavulana 39.
Tuhuma za wavulana kufanyiwa vitendo hivyo haramu ziliibuliwa Februari mwaka huu baada ya mvulana mmoja kutoa taarifa kuwa amekuwa akiingiliwa na mpishi ambaye amefanya kazi katika kituo hicho kwa miaka takribani kumi.
Mtoto huyo alieleza kuwa mpishi alikuwa akiwaita jikoni na kuwafanyia vitendo hivyo usiku na pia aliwatishia kuwa angewanyima chakula endapo wangemueleza mtu yeyote anachowafanyia.
Kwa mujibu wa Citizen, vipimo vya kitabibu vilivyofanywa katika Hospitali ya Machakos vimethibitisha kuwa mvulana huyo alikuwa akiingiliwa. Polisi wameanza kufanya uchunguzi zaidi kuhusu suala hilo wakimshikilia mpishi huyo.
-
Basi la shule latekwa na kuchomwa moto likiwa na wanafunzi 51
-
Video: Sababu ya wanawake wa kabila hili kutoboa midomo na kuweka visahani