Kiungo wa zamani wa Simba SC Shekhan Rashid ‘Zizzou’, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu usajili unaoendelea kufanywa na Uongozi wa Klabu hiyo katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya 2023/24.

Usajili wa Wachezaji wa Kimataifa Willy Onana na Aubin Akramo umempa nafasi Shekhan kufunguka kwa kina huku akiupongeza Uongozi kwa kufanya kazi kubwa ya kuwapata wachezaji hao wanaocheza zaidi ya nafasi moja dimbani.

Shekhan aliyetamba na Simba SC msimu wa 2001-2002 alisema amefuatilia usajili huo na kuridhika nyota wote wapya walioletwa na Mnyama wana rekodi nzuri huko walikotoka kwa kufanya vizuri na kuondoka na tuzo ikiwamo mfungaji bora, mchezaji bora na beki bora.

“Yes usajili huu utaleta impact (faida) kubwa sana kwa sababu wachezaji wote ambao wamesajili mpaka sasa walikua na season (msimu) nzuri na wame prove (dhihirisha) hilo kwenye timu walizotoka,” amesema Rashid aliyewahi pia kuzitumiakia Azam FC na Mtibwa Sugar.

David De Gea kurudi nyumbani Hispania
Mashujaa FC kuvuka Bahari ya Hindi