Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amewatoa wasiwasiwa wakazi wa Kigamboni, juu ya usafiri wa Vivuko ambavyo kwa sasa vinaonekana kuwa kero kwa abiria wa Manispaa hiyo na kwamba Serikali inaleta kivuko chenye uwezo wa kubeba abiria 3,000 na Magari 80 kwa wakati mmoja.

Naibu Waziri Kasekenya ametoa kauli hiyo wakati wa ukaguzi wa Kivuko cha MV Kazi ambacho kipo katika matengenezo huku akiwataka wasimamizi wa ukarabati huo kufanya haraka ili kuondoa usumbufu kwa abiria kutokana na kubaki na vivuko viwili.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri Kasekenya ukarabati wa kivuko ulitakiwa kutumia miezi minne lakini wamezungumza na Mkandarasi kupunguza muda huo badala yake kitakamilika baada ya miezi mitatu.

Aidha amesema kuwa kwasasa wapo katika mazungumzo ya kuongeza sehemu ya Maegesho ya magari na kutoa fidia kwa wakazi waliopo jirani na kivuko hicho, ambapo kwa sasa sehemu hiyo ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya magari yanayokuwa kwenye foleni ya kuingia ndani ya kivuko

Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 3,826
Rais Samia mgeni rasmi siku ya Vyombo vya habari