Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kassim Majaliwa, amewataka wakulima wa chai wilayani Lushoto wajiandae na kilimo hicho kwa kuwa kiwanda cha Mponde kilichopo katika jimbo la Bumbuli, kinatarajiwa kuanza uzalishaji hivi karibuni baada ya kusimama kwa muda mrefu.

Majaliwa ameeleza hayo wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto, mkoani Tanga katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Soni wakati akimuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli na wagombea udiwani  baada ya mgombea ubunge wa jimbo hilo January Makamba kupita bila kupingwa.

Majaliwa amesema hatua zote za msingi zimekamilika ambapo msimamizi mkuu ni msajili wa hazina na mwekezaji ni mifuko ya hifadhi ya jamii ya PSSSF na WCF ambao walishafanya ukaguzi.

Kiwanda cha chai cha Mponde ni miongoni mwa viwanda vya kusindika majani mabichi ya chai katika Halmashauri ya Bumbuli na hutegemewa na wakulima wadogo wa chai wapatao 5,000 kama soko la majani mabichi ya chai kutoka katika mashamba yao, ambapo uzalishaji ulisimama kufuatia mgogoro uliojitokeza mwaka 2013.

Azerbaijan na Armenia zakubaliana kusitisha mapigano
Covid 19 Ulaya bado kizungumkuti