Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa mapato yanayokusanywa katika bandari hiyo yameongezeka kwa asilimia 25 ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Deusdedit Kakoko amesema kuwa ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa ufanisi katika upitishaji wa mizigo.

Amesema kuwa kiasi cha sh. 420 bilioni kilikusanywa katika kipindi cha kati ya Julai na Desemba mwaka 2017 ukilinganisha na kiasi cha sh. 360 bilioni zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka 2016.

Aidha, katika mwezi Januari pekee, kiasi cha shilingi 72 bilioni zilikusanywa na Februari ni sh. 75 bilioni. Kiwango hicho kinatafsiri ongezeko la wastani wa makusanyo ya mwezi kutoka sh 60 bilioni Julai 2017 hadi sh 75 bilioni kwa Februari 2018,

Kakoko ameongeza kuwa sababu nyingine ya ongezeko hilo ni kuongezeka kwa mizigo inayoingia licha ya kupungua kwa idadi ya meli zinazowasili.

“Kupungua kwa idadi ya meli zinazoingia bandarini kunatokana na ukweli kwamba siku hizi meli moja inakuwa na uwezo wa kubeba mizigo ya takribani meli kumi,” alisema Kakoko.

Kakoko ameyasema hayo wiki hii ambayo ni wiki ya maadhimisho ya miaka 13 ya Mamlaka hiyo.

 

 

Serikali kuimarisha hali ya usalama nchini
Zesco kumthibitisha Lwandamina kama kocha mkuu