Mshambuliaji wa Man City Sergio Aguero huenda akaukosa mchezo ujao wa ligi kuu ya soka nchini England ambao utakunatisha na mahasimu wao wakubwa wa mjini Manchester, Man Utd Septemba 10.

Aguero yupo katika mashaka ya kuukosa mchezo huo kufuatia kitendo cha alichokifanya wakati wa mchezo wa jana dhidi ya West Ham Utd cha kumpiga kiwiko beki Winston Reid ambacho hakikuonwa na muamuzi.

Kitendo hicho kilifanywa na mshambuliaji huyo katika dakika ya 76 ya mchezo huo ambao ulimalizika kwa Man city kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja.

Kamati ya nidhamu ya chama cha soka nchini England FA, inatarajiwa kukutana na kulifuatilia tukio hilo kwa njia ya televisheni na kama watabaini ukweli wa tuhuma zinazoelekezwa kwa Aguero, huenda wakatoa maamuzi ya kumfungia michezo zaidi ya miwili.

Meneja wa West Ham Utd, Slaven Bilic alizungumza kwa uchungu alipokutana na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo na aliwataka waamuzi kuwa makini na matukio yanayofanyika uwanjani.

Hata hivyo kwa upande wa meneja wa Man City Pep Guardiola alidai kuwa, hakukiona kitendo hicho, hivyo hakutaka kuzungumza lolote katika mkutano na waandishi wa habari.

Finca yapongezwa kwa kupunguza gharama za ukopaji.
Polisi yasema Lema Kugoma Kula ‘ni Kosa la jinai’, Mwanasheria wake atangaza hatua