Watu wanne nchini Afrika Kusini wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili ya kula nyama ya binadamu, baada ya mmoja wao kujisalimisha katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama za binadamu.
Baada ya kufanyiwa mahojiano na polisi, mtu huyo alionyesha mguu na mkono wa binadamu hali iliyowashtua askali hao na kuamua kuongozana naye mpaka sehemu ambazo wanafanyia shughuli zao mtaa wa KwaZulu-Natal ambapo ilikutwa miili mingi ya binadamu.
Aidha, Polisi nchini humo walifanikiwa kuwakamata waganga wawili wa kienyeji na watu wengine wawili wanaojihusisha na ulaji wa nyama za binadamu, hivyo kuwafungulia mashtaka ya mauaji watu hao.
Mwezi mmoja uliopita mjini Durban, mtu mmoja alikamatwa akiwa na kichwa cha binadamu ambacho inasemekana alikuwa na mpango wa kukiuza kwa mganga wa kienyeji.
-
Msimamizi wa uchaguzi akutwa ameuawa nchini Kenya
-
Manowari ya Marekani iliyozama miaka 72 iliyopita yapatikana
-
Marekani, Korea Kusini zaungana kufanya mazoezi ya kijeshi
Hata hivyo, Polisi nchini humo wamesema kuwa uchunguzi bado unaendelea na wamewashauri wananchi kufuatilia ndugu zao waliotoweka huenda wakawa wameuawa na wahalifu hao.