Klabu ya Crystal Palace imeanza mazungumzo ya awali ya kumsajili kwa mkopo kiungo kutoka nchini England Jack Wilishere.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 amepata ofa kadhaa kutoka klabu za ndani na nje ya England baada ya Arsenal kukubali aondoke kwa mkopo wa muda mfupi, lakini Palace wanapewa nafasi kubwa kufuatia jana mchana Wilshere kufanya mazungumzo na kocha wa timu hiyo, Alan Pardew.

Wilshere atafanya maamuzi yake ya mwisho hii leo kabla ya dirisha la usajili wa majira ya kiangazi halijafungwa mishale ya saa tano na dakika hamsini na tisa (23:59) usiku kwa saa za England.

Timu mbili za Italia, AS Roma na Juventus pia zimeonesha nia ya kumchukua mchezaji huyo wa England, lakini ushindani mwingine umeongezeka kufuatia uwepo wa klabu kama Bournemouth na Watford za ligi kuu ya soka ya England, kuhitaji saini yake.

Taarifa nyingine zinadai kuwa, meneja wa Man City Pep Guardiola anatamani kuingia katika kinyang’anyiro hicho, lakini kikwazo kitakuwa kwa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye hawezi kukubali dili hilo kufanyika kutokana na klabu hiyo ya Etihad Stadium kuwa mpinzani mkubwa katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu.

Ikumbukwe kwamba, Arsenal imekua ikitajwa kuwa miongoni mwa klabu ambazo huenda zikaingia katika ushindani wa kuwania ubingwa msimu huu, hivyo Wenger anaamini kama atakubali kumuachia kiungo huyo kujiunga na Man City, itakua sawa na kumuuzia silaha mpinzani wake wa karibu.

Werder Bremen Wapinga Kuzidiwa Kete Na FC Bayern Munich
Jukwaa la wahariri lapinga kufungiwa Radio 5, Magic Fm