Klabu ya Yanga, imewatoa hofu mashabiki wa Jangwani kuwa kukosekana kwa nyota wao wanne katika kikosi kilichosafiri Mei 03, 2018 kuelekea Algeria kuwa hakiusiani na masuala ya mgomo wowote bali kimetokana na baadhi ya wachezaji hao kuwa majeruhi na majukumu ya kifamilia.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Dismas Ten baada ya kuzuka mjadala mkubwa kwa wapenzi wa soka nchini ambapo kila mmoja amekuwa akisema lake na wengi kuhusisha na suala ukosefu wa fedha ambalo linaonekana kuwa ni changamoto kubwa kwenye klabu hiyo kwa kipindi hiki.
“Kelvin Yondani na Papy Kabamba hawa wote bado majeruhi mpaka hivi sasa, waliumia katika michezo iliyopita na kusababisha hata katika ‘kariakoo derby’ wasiweze kucheza kwa kiwango chao, Ajib mke wake ni mjamzito na anatarajia kujifungua muda wowote kutoka sasa hivyo inampasa abaki kumuangalia mke wake. Obrey Chirwa anaumwa ugonjwa wa malaria kwa hivyo jana alilazimika kuondolewa katika kikosi kutoka na kuumwa kwake,”amesema Ten
Aidha, Kikosi cha Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, kimeshawasili mjini Algers nchini Algeria tayari kwa ajili ya kutupa karata yao ya kwanza hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao U.S.M Algers kesho jumapili Mei 06, 2018.
Hata hivyo, Kikosi kilichosafiri ya Yanga kina jumla ya wachezaji 17 akiwemo Youthe Rostand, Ramadhani Kabwili, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Said Juma Makapu, Raphael Daud, Juma Mahadhi.
Wengine ni Emmanuel Martin, Yusufu Mhilu, Pius Buswita, Yohana Mkomola, Geofrey Mwashiuya, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Andrew Vicent, Juma Abdul, Haji Mwinyi na Pato Ngonyani.
-
Rufaa ya Young Africans yawekwa kapuni
-
Kamati ya saa 72 yampiga STOP Kelvin Yondani
-
Manara awatoa hofu mashabiki wa Simba SC, ”nawezaje kuwaacha simba?”