Klabu ya Tottenham imeripotiwa kuingia katika vita ya kuwania saini ya beki wa OGS Nice, Jean-Clair Todibo anayefukuziwa na Liverpool na Manchester United.

Kocha Ange Postecoglou anataka kuboresha kikosi chake mwezi Januari 2024, baada ya kufunga mechi tatu mfululizo Ligi Kuu England.

Sasa kocha huyo ataingia sokoni kuangalia mchezaji gani anayeweza kufiti katika kikosi chake dirisha dogo mwezi Januari 2024.

Kwa mujibu wa ripoti, kocha huyo angependa kuongeza kiungo mwingine, mshambuliaji na beki huku Todibo akipendekezwa.

The Sun imedokeza kwamba kocha Postecoglou ana shaka juu ya hatma ya beki Eric Dier na endapo ataondoka, Todibo anaweza kuchukua nafasi.

Hata hivyo, Spurs itapata upinzani kutoka kwa Man United ambayo pia imeonyesha nia ya kumsajili beki huyo mwezi Januari 2024.

Todibo mwenye umri wa miaka 23, ambaye aliwahi kuichezea FC Barcelona, ameisaidia timu yake kujikita katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Ufaransa ‘Ligue 1’ kutokana na kiwango chake msimu huu 2023/24.

Mbali na beki huyo, Spurs imevutiwa na Marc Guehi kutoka Crystal Palace, Jarrad Branthwaite anayeichezea Everton na Lloyd Kely wa Bournemouth.

Lakini bei ya uhamisho wa Todibo imekuwa chaguo bora katika soko la usajili ndo mana timu nyingi zinavutiwa naye.

Viongozi, Wachezaji Simba SC waweka maazimio
Kamwe: Waarabu hawataamini kitakachowakuta