Meneja mpya wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amekiangalia kikosi chake cha sasa kasha amekuja na kauli moja kwamba lazima aingie sokoni kwa ajili ya kumsainisha mlinda mlango wa kiwango cha kuisaidia timu.

“Nikizungumzia suala la usajili wa majira ya baridi bila kuweka malengo madhubuti nitakuwa ninazichezea akili za wanaoipenda Liverpool.”

“Ninahitaji kufanya usajili mdogo lakini ulio na maana kwa ajili ya klabu na eneo ambalo nalitazama kwa macho mawili ni idara ya mlinda mlango.”

“Lakini sio mlinda mlango tu, bali ni lazima niwe na muda wa kuangalia vigezo na viwango ili mwisho wa siku nipate mlinda mlango aliye bora,” alisisitiza Klopp.

Hatua hiyo inakuja baada ya kuiongoza timu yake katika mechi chache za Ligi na kuona eneo analoliona linapwaya ni la ulinzi, kuanzia katika nafasi ya mlinda mlango.

Hatua ya kocha Klopp kuzungumzia hilo linakuja siku chache baada ya kukaa siku chache, lakini amesisitiza mpango wake wa kusajili upo palepale.

“Nitakamilisha usajili wa mlinda mlango wa maana katika usajili ujao wa mwezi Januari mwakani, kwasababu tunahitaji kusuka kikosi bora cha ushindani ndani na nje ya Ligi ya premier inayoendelea.”

“Nafikiri tunahitaji mlinda mlango wa kiasi kikubwa, inategemea na aina ya mahitaji tuliyonayo kwa sasa,” alisema Klopp.

Alisema kuwa, kwa vyovyote bado wapo chini, wana walinda mlango vijana nyuma na wanahitaji kuangalia maendeleo ya klabu.

“Sisi ni kati ya klabu kubwa hivyo hata aina ya wachezaji lazima wawe bora kulingana na ukubwa wa timu tuliyonayo.”

“Ninaweza nikaficha ukweli huu sasa lakini baadae ninaweza nikajisuta mwenyewe kama nitaendelea kujiaminisha kuwa tuna kikosi bora. Hapana, tunahitaji wengi walio bora akiwemo mlinda mlango,” amesisitiza Klopp abaye ni kocha wa zamani wa Borussia Dotmund ya Ujerumani.

Mkwasa Amkabidhi Kitambaa Cha Taifa Stars Samatta
Man City Yabisha Hodi Ujerumani