Aliyekua meneja wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya Olympic Marseille, ambayo kwa sasa haina mkuu wa benchi la ufundi baada ya kujuzulu kwa Marcelo Bielsa.

Bielsa alijiuzulu mwishoni mwa juma lililopita mara baada ya mchezo wa kwanza wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa.

Wakala wa meneja huyo kutoka nchini Ujerumani, Marc Kosicke amesema viongozi wa klabu ya Olympic Marseille waliwasilisha ofa ya kutaka kumpa ajira Klopp, lakini mkakati huo umeshindikana.

Kosicke, amesema suala hilo limeshindikana kufuatia msimamo wa mteja wake wa kuhitaji kupumzika kama alivyoahidi mwishoni mwa msimu uliopita alipokua akiachana na klabu ya Borussia Dortmund ambayo aliitumikia kwa mafanikio makubwa.

Klopp aliiwezesha klabu ya kutwaa mataji mawili ya ligi ya nchini Ujerumani, kombe la chama cha soka nchini humo mara moja, ngao ya jamii mara mbili pamoja na kuifikisha klabu hiyo kwenye mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Marcelo Bielsa, ambaye ni raia wa nchini Argentina aliwashangaza wengi mwishoni juma lililopita, pale alipotangaza kuachia ngazi kwenye klabu ya Olympic Marseille mara baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Caen.

Real Madrid Kumrudisha Cheryshev
Tetesi Za Usajili Barani Ulaya