Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amejibu kejeli zilizoelekezwa kwa timu yake na mpinzani wake, Kocha msema mengi, Jose Mourinho wa Man Utd aliyedai kuwa timu hiyo haina budi kunyakuwa ubingwa msimu huu kutokana na kuvunja rekodi ya uwekezaji.

Mourinho alidai kuwa Liverpool ndio washiriki wakubwa zaidi msimu huu kwa kuwa wametumia £170 Milioni kwa ajili ya usajili wa wachezaji wanne katika dirisha la msimu wa kiangazi.

Kocha huyo aliendelea kushindilia msumari wa kejeli akieleza kuwa Liverpool imeweka rekodi kwenye msimu huu baada ya kutumia takribani £250 milioni katika kipindi cha miezi 12. Hivyo ‘wanastahili’ kubeba ubingwa.

“Sioni kama kuna timu yoyote ambayo inasogelea uwekezaji ule. Timu ambayo ilimaliza kileleni mwa ligi ya mabingwa, unatakiwa kusema ndio washiriki wakubwa. Wanapaswa kushinda,” alisema.

Kejeli hizo zimejibiwa na Klopp aliyedai kuwa moja kati ya malengo yake makuu mwaka huu ni kuhakikisha anamfanya Mourinho ‘atabasamu’.

“Hii ni dunia huru na mimi sina tatizo lolote na Jose,” alisema Kocha huyo kutoka Ujerumani. “Sisi tuna jukumu kwa mashabiki wetu na mmiliki wa timu yetu na sio kwa mtu mwingine yeyote. Mimi sina nia yoyote dhidi ya Man Utd,” aliongeza.

Akiangalia kwa jicho la tatu mtego wa maneno aliyowekewa na Mourinho, Klopp alihoji, “kwahiyo [nisiposhinda] nitimuliwe? Hii inategemeana na mpira tunaocheza.”

Liverpool walimsajili kiungo Naby Keita kutoka Monaco kwa zaidi ya £40 milioni, winga kutoka Uswisi Xherdan Shaqiri alivutwa kwa kitita cha £13 milioni.

Hata hivyo, Klopp amedai alisema kuwa hii haimaanishi kuwa wapinzani wao walikuwa wamelala kwahiyo hawawezi kujihakikishia ushindi kabla ya pambano.

Video: Pangapangua ya JPM ilivyowapa shavu Jokate, Muro, Kafulila, Katambi
Waitara ang'oka Chadema, adai Mbowe ni tatizo