Meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp, amepuuza uvumi wa kuvunja rekodi ya kuwa meneja atakaekaa kwa muda mrefu zaidi katika ligi ya nchini England, rekodi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Arsene Wenger wa Arsenal.
Meneja huyo kutoka nchini Ujerumani amesema miaka 20 ijayo atakuwa na umri wa miaka 70 na amewahikikishia mashabiki wa Liverpoolkuwa, hatakuwepo klabuni hapo kama inavyozungumzwa na baadhi ya vyombo vya habari na kwenye mitandao yakijamii.
Klopp alisaini mkataba wa miaka sita wa kukinoa kikosi cha Liverpool mwaka 2016, ambao utaisha 2022, lakini haamini kama ana nafasi ya kufikia rekodi za Arsene Wenger ama Sir Alex Ferguson (mejena wa zamani wa Manchester United.
Amesema kuna tofauti kubwa sana ya mameneja wa zamani ambao walikuwa kwenye utulivu, tofauti na soka la sasa hivi ambapo limejaa shinikizo kutoka kila kona.