Aliyekua meneja wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amevitahadharisha vyombo vya habari kutotarajia makubwa katika maamuzi atakayoyafanya mwishoni mwa msimu huu.

Klopp ambaye kwa sasa yupo pembeni kwa kisingizio cha kupumzika ametoa tahadhahi hiyo baada ya kuandikwa sana katika baadhi ya vyombo vya habari hukua kihusishwa kuwa na mipango ya kuajiriwa kwenye klabu kubwa.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 48 amekua akitajwa kuwa katika harakati za kusubiri bahati yake ya kupata ajira katika kipindi hiki cha msimu wa 2015-16, endapo klabu yoyote kubwa itafanya maamuzi ya kumtimua meneja wake.

Tayari imeanza kuhisiwa huenda Klopp anaitamani nafasi ya kuwa kiongozi wa benchi la ufundi la Real Madrid kutokana na meneja wa sasa wa klabu hiyo kuonyesha kutokua na mvuto kwa mashabiki.

Klopp pia alihushwa na mkakati wa kuchukua ajira ya meneja wa Man city Manuel Pellgrini lakini siku chache baadae mzee huyo kutoka nchini Chile aliongezewa mkataba wa kuendelea kufanya kazi huko Etihad Stadium.

Klopp aliomba kusitishiwa ajira yake Signal Iduna Park mwishoni mwa msimu uliopita, kwa kutoa sababu za kuhitaji kupumzika kwa msimu mmoja na kisha atarejea tena katika tasnia ya ufundishaji.

 

Iceland, England, Czech Republic Zatangulia Ufaransa
Samatta Ajimilikisha Ulaya