Kocha wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amesema winga mpya Alex Oxlade-Chamberlain aliyesajiliwa na klabu hiyo kutoka Arsenal anahitaji muda ili kuzoea na kuendana na mtindo wa uchezaji wa Liverpool.

Chamberlain aliyesajiliwa kwa kiasi cha Pauni milioni 40 kutoka Arsenal atapangwa katika kikosi cha Liverpool kinachotarajia kupambana na Leicester City leo katika mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa King Power.

Mchezaji huyo amecheza kwa jumla ya dakika 57 tu akitokea benchi katika michezo yote mitatu aliyoichezea Liverpool mpaka sasa.

Kocha Jurgen Kloop amesema anafurahi kuwa na Chamberlain kwenye kikosi chake na mchezaji huyo hakufanya makosa kujiunga na Liverpool japo amekuwa akitokea benchi katika michezo mitatu iliyopita, na kadri muda unavyokwenda atazoea mtindo wa uchezaji wa Liverpool na kuingia katika kikosi cha kwanza.

”Chamberlain ni mchezaji mzuri tunakaa naye kumuelekeza ni mtindo gani na nafasi gani tunataka acheze na hilo halihitaji haraka atapiga hatua kubwa”, alisema Klopp.

Chamberlain alijiunga na Arsenal mwaka 2011 na ameichezea klabu hiyo jumla ya michezo 132 na kufanikiwa kufunga mabao 9.

Mlinda amani raia wa Tanzania auawa nchini Congo
Lissu ampa ujumbe mzito Zitto, ‘Tumeshinda’