Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa leo kikosi chake kitapata tabu mbele ya kisiki cha msitu wa Barcelona kwenye mechi ya nusu fainali ya Klabu Bingwa Barani Ulaya lakini watakuwa na nafasi pia ya kuwika.
Klopp ambaye mwaka jana aliwaongoza Majogoo hao wa London kuingia Fainali za kombe hilo amesema, “itakuwa ngumu sana kwetu leo, lakini itakuwa inavutia zaidi tukipata nafasi.”
Liverpool na Barcelona wote wana historia ya kushinda mara tano kombe hilo. Barcelona wao ushindi wao umekuja katika kipindi cha miaka 13 iliyopita, wakati Liverpool hesabu zao ni za zamani na walishinda tena kwa mara ya kwanza mwaka 2005 tangu walipobeba mwaka 1984.
Moto wa Barcelona hivi sasa uko juu kwani wameshinda mechi 31 mfululizo za nyumbani.
“Ukiuliza kama tutakuwa wakamilifu? Hiyo haiwezekani. “Je, tutafanya makosa?’ Oh, ndio. ‘Tutapata tabu?’ Oh, ndiyo, 100%. ‘Kutakuwa na wakati ambao tutapata nafasi?’ Ndiyo, 100%. Ninatumaini tutazitumia nafasi hizo na hayo ndiyo tutakayojaribu kufanya,” alisema Klopp.
“Tunaweza kujisikia huru kucheza mchezo wetu. Ninaweza kusema sare haitakuwa matokeo mabaya kuliko yote duniani, sio kwamba ndiyo tunayoyafuata lakini yatakuwa poa,” aliongeza.
“Watu wengi wamekuja hapa Barcelona na walikuwa na mipango/mikakati lakini mwisho wa siku wakapigwa vizuri tu,” alisisitiza.
Mtanange wa leo una msisimko wa aina yake ikiwa ni mechi ya kwanza ya nusu fainali kati ya timu hizo. Je, majogoo wa London watawika ugenini? Muamuzi dakika 90.