Kocha mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amewataka mashabiki wa timu yake kuyaamini maamuzi ya kutomsajili Alex Teixeira kutoka Shakhtar Donetsk katika kipindi cha majira ya baridi.

Klopp ambaye ametua Liverpool kuchukua nafasi ya Branden Rodgers aliyefungashiwa virago amesema ni muhimu kuamini uamuzi waliofanya.

“Ni muhimu sana endapo mutatuamini. Yalikuwa maamuzi ya kawaida juu ya Teixeira. Tulisema hatuwezi kucheza mchezo huu mpaka mwisho” alisema.

Licha ya kutotaka kuzungumzia sana juu ya suala hilo, Klopp amesema wakikuwa wakweli kuhusu majumuisho hayo kufanyika mwezi Januari.

Jurgen Klopp and Alex Teixeira

“Tuliweka ofa, siwezi kulisemea sana hilo, lakini walikuwa wakweli kwa majumuisho hayo kufanyika mwezi Januari.

“Lakini ikikuwa kesi ya ‘Kama hutaki Sawa, hatuwezi kubadilisha hali kivyovyote sasa na baadae.

“Si kwamba hatukuwa na pesa lakini unatakiwa kufanya kazi kiufasaha zaidi na kuwajibika zaidi. Ndivyo tunavyofanya” alisema Jurgen Klopp.

Usajili mkubwa uliofanywa na Liverpool katika dirisha hili la usajili ni kwa mlinzi wa kati wa QPR, Steven Caulker aliyesajiliwa kwa mkopo.

Floyd Mayweather Atoboa Siri Ya Ushawishi Wa Pesa
Friends Rangers Wapiga Hesabu Za Kuwafuata Ruvu Shooting