Meneja wa Majogoo wa Jiji ‘LIVERPOOL’ Jurgen Klopp hana mpango wa kuziba nafasi za Washambuliaji wake kutoka Afrika wakati wa Dirisha Dogo la Usajili mwezi Januari 2022.

Wachezaji Mohamed Salah, Sadio Mane na Naby Keita wataondoka kwenye kikosi cha Liverpool mwezi Januari 2022, kwenda kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa karibu mwezi mzima.

Klopp amesema anafahamu wachezaji hao watatu wataondoka na kurejea Afrika, lakini anakiamini kikosi chake ambacho kitaendelea kuwa na wachezaji mahiri, ambao wataweza kuziba nafasi zitakazoachwa wazi.

Amesema kutokana na kuamini huko, haoni sababu ya kuingia sokoni Mwezi Januari 2022, kwa kisingizio cha kumsaka mchezaji ama wachezaji ambao wataongeza chachu ya kusaka mafanikio kwenye michezo itakayowakabili kwa mwezi huo.

“Ni vigumu kuziba nafasi zao,” amesema.

“Tulijua watatu wangefuzu na kuwepo, na tulijua kwamba angalau wawili kati yao watafika mbali sana kwenye dimba,” amesema Klopp.

“Je, unaweza kuwa tayari kwa kitu kama hicho, vizuri, kikamilifu? Kama mbadala wa Sadio, badala ya Mo, badala ya Naby? Hilo ni gumu katika kila hali lakini nina furaha na kikosi na tuna chaguzi za kucheza na bado kucheza soka la ushindani na tukapata ushindi.” Klopp amesisitiza kabla ya mchezo kati ya timu yake dhidi ya Newcastle utakaopigwa kwenye Uwanja wa Anfield leo Alhamisi (Desemba 16) usiku.

Michuano ya AFCON inaning’inia huku waandaaji wakisisitiza kuwa bado itafanyika licha ya ripoti zilizoenea kwamba huenda ikalazimika kutupiliwa mbali kutokana na janga la virusi vya Omicron linaloenea kwa kasi.

Wakurugenzi wapigwa marufuku kuwashusha vyeo wakuu wa shule
Simba waongeza mzigo ASFC