Meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amebainisha kwamba, wachezaji wake wapo tayari kwa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester City katika michezo 10 iliyobaki kabla ya kufika mwisho wa msimu huu 2021/22.

Wapinzani hao wamekuwa wakikimbizana kwenye ubingwa wa ligi hiyo tangu msimu wa 2018-19 wakati Man City ilipotwaa ubingwa ikiwa na alama 98, moja zaidi ya Liverpool ambayo ilipoteza mchezo mmoja tu.

Alipoulizwa kuhusu mbio hizo, Klopp aliiambia BT Sport: “Hatuwezi kuepuka hilo.”

Meneja huyo kutoka nchini Ujerumani anajua namna Ligi ilivyo ngumu kuikabili Man City, lakini licha ya pengo lililoko anaamini Liverpool wana nafasi kwenye mbio hizo.

Liverpool watasafiri kwenda kwenye dimba la Etihad kuwavaa Man City mwezi ujao kwenye ligi hiyo.
“Unawatarajia wao kushinda mechi wakati unapowaona wanapocheza,” amesema Klopp.

“Kwa sababu tupo nyuma yao, naamini tuna nafasi kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu. Jambo pekee la msingi ni kuhakikisha tunashinda mechi zetu zote.”

Bikra mwenye miaka 56 anatafuta mchumba
Mashabiki Simba SC wapewa shukurani, wapongezwa