Kikosi cha KMC FC kitashuka Dimbani Jumamosi (Februari 05) kuikabili Biashara United kutoka mkoani Mara katika mchezo wa Mzunguuko wa 14 wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22.

Awali mchezo ulipangwa kuunguruma keshokutwa Ijumaa (Februari 04) Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, utaanza mishele ya saa 10:00 jioni, na umehamishiwa Uwanja wa Azam Complex.

Kwa mujibu taarifa iliyowasilishwa kwetu na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya KMC FC imeeleza kuwa, uongozi wa klabu hiyo umepokea barua ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), ikieleza mabadiliko hayo, ambayo yametokana na kuwepo kwa ukarabati wa miundombinu ya uwanja wa Uhuru ambao unaendelea kwa sasa.

Aidha barua hiyo pia imeeleza kuwa siku hiyo ya Ijumaa (Februali 04) katika Uwanja wa Azam Complex pia kutakuwa na shughuli nyingine ikiendelea na hivyo kuamua kuusogeza mbele mchezo huo siku ya Jumamosi.

“Klabu ya KMC imepokea kwa mikono miwili mabadiliko hayo na kwamba mashabiki ambao walikua wamejiandaa kwa ajili ya kushuhudia burudani safi kutoka kwa vijana wa Kino Boys kwenye uwanja wa Uhuru wajiandae kwa ajili ya kwenda kuwasapoti kwenye uwanja wa Azam Complex kama ambavyo barua ya TPLB Ilivyo elekeza.”

“ Tumeona ni muhimu kuwapa taarifa hii mapema mashabiki zetu ilikuepusha usumbufu kwani tunafahamu wengi walijiandaa kuja Uhuru, lakini niwasihi kwamba tujiandae kuwasapoti vijana wetu siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Azam Complex, kama Timu tumejipanga vizuri lakini pia mabadiliko yamekuja kwa wakati hivyo hayawezi kuathiri mchezo wetu kikubwa tujitokeze kwa wingi uwanjani.” Imeeleza taarifa hiyo

Kwa upande wa maandalizi ya kikosi cha KMC FC, Idara ya habari inayoongozwa na Christina Mwagala, imesema maandalizi ya kuelekea mchezo huo yanaenda vizuri na kwamba wachezaji wanamorali kuelekea kwenye mchezo huo kwa lengo la kuhakikisha kwamba kama Timu tunakwenda kupata ushindi licha ya ushindani mkubwa utakaokuwepo.

“Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thiery Hitimana inaendelea kujifua kwani mchezo huo ni muhimu kwa ajili ya kuhitaji ushindi ili kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC ambapo kwa sasa KMC ipo kwenye nafasi ya 10 ikiwa imeshacheza michezo 13 na kukusanya jumla ya alama 15.”

“Kwenye mchezo wetu wa Jumamosi tunahitaji kufanya vizuri, tunakutana na Biashara ambayo nao pia wanahitaji kupata matokeo ,na ukiangalia kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC tunatofautiana alama Nne, hivyo tutakwenda kupambana ili kuondoka na alama tatu muhimu siku hiyo kwakuwa mchezo huo upondani ya uwezo wetu lakini pia uimara wawachezaji pamoja na benchi la ufundi tulionao unatupa nafasi hiyo ya kufanya vizuri.

TZ Prisons yajihami kuikabili Simba SC
Mhadhiri chuo kikuu Michigan Marekani ateuliwa kuwa balozi kutangaza utalii wa Tanzania