Kocha wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC Habibu Kondo amesea kuwa licha ya kupoteza mchezo dhidi ya Tanzania Prisons bado anakiamini kikosi chake kitaibuka na ushindi katika mchezo wa kesho na hivyo kuondoka na alama tatu dhidi ya Mwadui FC.

Habibu amesema kuwa mchezo wa kesho hauwezi kuwa mgumu kwa kwasababu anaifahamu Mwadui licha ya kwamba wapovizuri lakini anaipa asilimia 100 KMC kupata matokeo mazuri kutokana na maandalizi ambayo yamefanyika hadi sasa.

Ameongeza kuwa kila Timu hivi sasa inahiaji alama tatu muhimu na kwamba KMC inayohitaji ushindi zaidi ili iweze kutimiza malengo yake na hivyo hana hofu katika mchezo wa kesho.

“Mwadui ni Timu nzuri lakini KMC ni bora zaidi, tumetoka kupoteza mchezo wetu tukiwa ugenini hivyo tutakwenda kuutumia vizuri uwanja wetu wa nyumbani katika mchezo wetu wa kesho ili alama tatu tuweze kubaki nazo” amesema Kocha Habibu.

KMC FC iilirejea Jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Februali 13 ikitokea Sumbawanga Mkoani Rukwa ambapo ilikwenda kwa ajili ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Nelson Mandela.

Hadi sasa KMC FC ipo kwenye nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara ikiwa na alama 25 ambapo hadi sasa imeshacheza michezo 19.

Imetolewa na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mahusiano wa Timu ya KMC FC.

Wakili wa Ruto aula ICC
Wahamiaji haramu wakamatwa wakielekea Dar kutafuta kazi