Mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara wa KMC FC dhidi ya Simba utapigwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Julai saba mwaka huu na kwamba kikosi hicho hivi sasa kinaendelea kujifua kuelekea katika mtanange huo.
KMC FC ambao ni wenyeji wa mchezo huo wanaendelea kujifua chini ya Makocha ,Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na Habibu Kondo kwa lengo la kuhakikisha kwamba Timu inakwenda kupata matokeo mazuri.
Licha ya kuwepo kwa ushindani mkubwa katika mchezo huo lakini uongozi pamoja na wachezaji umedhamiria kupata alama tatu kwakuwa KMC FC haijawahi kushindwa na kwamba itahakikisha ushindi huo unapatikana ili kuendelea kujiweka katika hatua nzuri ya kuendelea kuwania nafasi ya Nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu 2020/2021.
“Tunafahamu mchezo huu utakuwa na ushindani mkubwa sana, kutokana na Timu ambayo tunakutana nayo imekuwa ikifanya vizuri, lakini Makocha wetu wanaendelea kukiweka vizuri kikosi cha wana Kino Boys kuwa bora kwa maana ya kupata alama tatu, nakumaliza kwenye nafasi nzuri, hivyo hatuna wasiwasi na mchezo huo kikubwa tunajenga tahadhari ikiwa ni pamoja na kuendelea kujiweka vizuri kabla ya Julai saba.
Katika hatua nyingine KMC FC leo imecheza mechi ya kirafiki dhidi ya Timu ya Pamba ya Mkoani Mwanza katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na kupata ushindi wa magoli mawili kwa sifuri ambayo yamefungwa na wachezaji Kelvin Kigili pamoja na Clifu Buyoya ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kujiweka sawa katika mchezo dhidi ya Simba.
Nugaz: Young Africans hatudhulumu
KMC FC kwa sasa imesalia na micheo mitatu kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu ambayo ni dhidi ya Simba, JKT Tanzania pamoja na Ihefu huku ikiwa imecheza michezo 31 na kujikusanyia jumla ya alama 42.
Imetolewa leo Juni 29
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mahusiano wa Klabu ya KMC FC