Kikosi cha KMC FC kinaendelea kujifua katika mazoezi yake ikiwa ni katika hatua ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara inayoanza Septemba sita mwaka huu.

Katika msimu huo wa ligi, timu ya KMC FC itaanza mchezo wake wa kwanza siku ya Jumatatu Septemba saba mwaka huu katika Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo itakuwa wenyeji wa mchezo huo dhidi ya Mbeya City kutoka Mkoani Mbeya.

Kocha wa timu hiyo, Habibu Kondo amesema kuwa kikosi chake kipo vizuri na kwamba wapo tayari kwa mtanange huo katika kuhakikisha kuwa wanakuwa mabingwa kwenye msimu wa ligi 2020/2021 .

Ameongeza kuwa katika maandalizi hayo wameweza kuboresha kikosi hicho ikiwa ni pamoja na kurekebisha changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita na kwamba katika msimu huu timu hiyo imekuwa na maboresho makubwa.

Amefafanua kuwa katika maandalizi hayo timu hiyo imecheza michezo ya kirafiki nane ambayo ni dhidi ya timu za DTB Bank, Kagera sugar, Namungo, JKT Tanzania, Polisi Azam pamoja na Simba na zimemsaidia katika maandalizi.

Balozi Kijazi: Wahandisi mjipange
Kigoma : 146 mbaroni kwa ujambazi, mauaji

Comments

comments