Kikosi cha KMC FC kimekamilisha maandalizi ya kuelekea mchezo wa mzunguuko wa 14 wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Dodoma Jiji FC utakaochezwa kesho Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

KMC FC wanaotamba na ‘Pira Spana’ kesho watakua nyumbani huku wakichagizwa na ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata mbele ya Azam FC majuma mawili yaliyopita, Uwanja wa Uhuru.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino KMC FC, Christina Mwagala amesema kuwa wachezaji wamepewa mbinu nyingi na makocha wao wawili ambao ni wazawa, jambo linalowapa matumaini ya kupata pointi tatu.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Uhuru kushuhudia Pira Spana kutoka kwa KMC, mbinu za John Simkoko ambaye ni Kocha Mkuu na Habibu Kondo zitaonekana ndani ya uwanja,” amesema Christina.

Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa KMC kuikaribisha Dodoma Jiji FC kwa kuwa imepanda daraja msimu huu wa 2020/21.

Tayari Dodoma Jiji FC wameshawasili jijini Dar es salaam tangu jana, wakitokea Dodoma, huku wakiwa na matumaini ya kupambana na kuondoka ugenini wakiwa na furaha.

KMC ikiwa nafasi ya 8 na pointi 18 baada ya kucheza mechi 11 inakutana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 9 na pointi 16 ikiwa imecheza mechi 12.

Simba SC yaikasirisha TFF
Masau Bwire amkosoa Haji Manara

Comments

comments