Kikosi cha KMC FC kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Young Africans ambao unatarajiwa kupigwa Aprili 10, kwenye Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar.

KMC FC imekuwa kwenye kiwango bora msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara ikishinda michezo 10 kati ya 24 walizoshuka dimbani ikishika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi hiyo.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Habib Kondo amesema: “Kikosi tayari kimeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi yetu na Yanga na mechi za Kombe la Shirikisho, malengo yetu ni kufanya vizuri kwenye mechi zetu zote zilizosalia ili tuweze kumaliza kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.

“Ushindani kwenye ligi umeongezeka ukizingatia kila timu inapambana kumaliza kwenye nafasi nzuri hivyo ni lazima tufanye maandalizi ya kutosha ili tuweze kufanya vizuri kwenye kila mechi ikiwemo mechi yetu dhidi ya Young Africans.

Mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa kwanza ulizikutanisha timu hizo jijini Mwanza, Uwanja wa CCM Kirumba ambapo KMC FC waliokua wenyeji walikubali kufungwa mabao 2-1.

Rais Samia aviwashia moto 'vifurushi'
Young Africans yabadili 'GIA' angani