Uongozi wa KMC FC  umeamua kuachana na mastaa wao 11 ambao wataenda kutafuta changamoto mpya nje ya timu hiyo, huku ukianza kukisuka kikosi bora kwa ajili ya msimu ujao wa 2023/24.

Ikumbukwe kuwa KMC FC walibakia Ligi Kuu baada ya kushinda mechi zao za Play Off dhidi ya Mbeya City ambao wameangukia kwenye Ligi ya Championship, kufuatia kufungwa na Mashujaa FC ya Kigoma.

Afisa Habari wa KMC FC, Christina Mwagala amesema: “Ni kweli tumeachana na mastaa 11 kwa lengo la kusajili wachezaji wengine ambao mwalimu kapendekeza na wachezaji ambao tumeachana nao wote tumeshawapa barua zao, kila mchezaji anafahamu kuwa hatakuwepo msimu ujao.

“Wachezaji ambao tumewaacha ni Erick Manyama, Steve Nzigamasabo, Mohamed Samata, David Kisu Mapigano, Nurdin Balora, Isaac Kachwere, Ally Ramadhan ‘Oviedo’, Abdul Hillary, Frank Zakaria na Denis Richard.

“Tunawashukuru kwa mchango wao mkubwa wa msimu wa 2022/2023 ambao walitusaidia kupambana mpaka kubaki ligi kuu baada ya kucheza playoff na Mbeya City.”

Sillah azichimba mkwara Simba SC, Young Africans
Jiheshimu: Mitandao si Mahakama, Ustawi wa jamii