Kikosi cha Manispaa ya Kinondoni, KMC FC (Kino Boys) kimeanza maandalizi ya mchezo wa mzunguuko watatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC, utakaochezwa Mkoani Shinyanga Septemba 21 mwaka huu.

KMC FC itakutana na Mwadui katika uwanja wa Mwadui Complex ambapo itakuwa ugenini dhidi ya mchezo huo huku ikihitaji ushindi kwa lengo la kuendelea kujiweka katika nafasi ya kuongoza ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2020/2021.

Kupitia mazoezi hayo kikosi hicho kitaendelea kujiimarisha  zaidi  kwa kucheza michezo ya kirafiki kabla ya kukutana na Mwadui FC, jambo ambalo litaiwezesha kujiweka tayari katika mchezo huo.

KMC FC hivi sasa inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama sita na magoli sita  katika michezo yake miwili ambapo Septemba saba, ilikutana na Mbeya City katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa goli nne kwa nunge, Septemba 12 ilicheza na Tanzania Prisons na kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja.

Tanzania: Mataifa 15 kupata kibali cha Uangalizi Uchaguzi mkuu
Wamiliki wa 'pool table' waagizwa kujisajili

Comments

comments