Idara ya Habari na Mawasilino ya KMC FC, imetoa taarifa ya muelekeo wa kikosi cha klabu hiyo baada ya kupoteza mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22, kwa kufungwa mabao 2-0 na Polisi Tanzania jana Jumatano (Septemba 29), mjini Karatu kwenye uwanja wa Black Rhino.

Mkuu wa idara hiyo Christina Mwagala amesema, nguvu ya kikosi chao kwa sasa inaelekezwa kwenye mchezo wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu, ambapo wataendelea kuwa ugenini kwa kuikabili Coastal Union ‘Mangushi’ ya jijini Tanga.

Mwagala amesema mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga wanaupa umuhimu mkubwa, ili kufanikisha lengo la kupata alama tatu muhimu ugenini kama ilivyokua jana Jumatano (Septamba 29), lakini mambo yaliwaendea kombo.

“Tumepoteza mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Polisi Tanzania, tunajipanga kwa mchezo wetu wa pili dhidi ya Coastal Union ambao tutaucheza ugenini pale Tanga, dhamira yetu kubwa ni kupambana na kupata alama tatu za mchezo huo ambao bado tunaamini utakua mgumu,”

“Jana Jumatano tulijipanga kupata ushidni mbele ya Polisi Tanzania lakini bahati haikuwa kwetu, benchi la ufundi limejifunza kutokana na makosa yaliyofanywa na wachezaji wetu, hivyo nguvu zinaelekezwa kwa Coastal Union.” amesema Christina Mwagala

Mchezo huo umepangwa kuchezwa keshokutwa Jumamosi (Oktoba 2), katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Coastal Union nao watahitaji kusaka alama tatu muhimu za mpambano huo, baada ya kulazimisha matoeko ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC.

Chui ajeruhi wanne mkoani Kilimanjaro
Bomba la mafuta kuwaneemesha wazawa