Uongozi wa Klabu ya KMC FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara umetangaza rasmi kuvunja Mkabata na Kocha Mkuu Thiery Hitimana pamoja na Benchi lake la ufundi kutokana na mwenendo mbovu wa matokeo katika timu hiyo.

KMC FC imetoa taarifa rasmi katika vyanzo vyake vya habari na kuthibitisha kuachana na Kocha huyo kutoka nchini Burundi, ambaye mwanzoni mwa msimu huu alikua na mwenendo mzuri wa matokeo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa nafasi ya Kocha Mkuu KMC FC kwa sasa inashikwa na Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye atakiongoza kikosi cha klabu hiyo hadi Mwishoni mwa Msimu huu.

“Bodi ya timu ya manispaa ya kinondoni [KMC FC] baada ya kukaa kikao mapema Leo asubuhi imeamua kuvunja benchi lote la ufundi lililokuwa likiongozwa na Kocha THIERY HITIMANA baada ya kufikia makubaliano kutokana na kutokulidhishwa na mwenendo wa Timu msimu huu.”

“Hivyo Basi, Uongozi umefikia makubaliano na Kocha JAMHURI KIHWELO JULIO ambae atachukua timu akiwa na benchi lake la Ufundi.” Imeeleza taarifa ya KMC FC

KMC inashika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 26, ambapo katika michezo 5 ya mwisho ya ligi imeshinda mchezo mmoja pekee, ikifungwa michezo 4.

Bodi za wadhamini 743 zakalia kuti kavu, RITA yataka zijieleze
Ben Chilwell achekelea mkataba mpya Chelsea