Klabu ya KMC FC imesaini mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Kusambaza vifaa vya michezo Duniani, MASITA SPORTS WEAR ya Nchini Uholanzi kwa ajili ya kusambaza vifaa vya timu kwa miaka miwili.

Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Agosti 11), chini ya Kampuni ya Level Up ambao ndio wawakilishi wenye hati miliki ya kusambaza vifaa vya MASITA kwa ukanda wa Africa Mashariki na Kati.

Katibu Mkuu wa KMC FC Mr Walter Harson amesema MASITA ni kampuni bora na wanategemea ubora zaidi utaongezeka baada ya kufanya kazi kwa msimu uliopita kwa kiwango kikubwa.

Awali wakisaini mkataba huo , Mkurugenzi Mtendaji wa Level Up Mr Daud Aboud amesema ni nafasi kubwa kwao kufanya kazi na timu kubwa kama KMC FC na wana imani watashirikiana vizuri katika makubaliano hayo na hivyo kutimiza malengo ya kuhakikisha wanaleta vifaa bora vinavyotengenezwa na kampuni hiyo ya MASITA.

Mkurugenzi Mtendaji wa Level Up Daud Aboud akisaini mkataba wa makubaliano ya usambazaji wa vifaa vya michezo ya KMC FC kwa kipindi cha miaka miwili.
Mwenyekiti wa Timu ya KMC FC , Kheri Misinga wapili kulia , Mkurugenzi Mtendaji wa Level Up, ndugu. Daudi Aboud watatu katikati wakiwa wameshika mkataba wa Makubaliano ya usambazaji wa vifaa vya michezo ya KMC FC uliosaniwa leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa KMC FC Walter Harison akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Level Up ,Ndugu. Daud Aboud wakiwa wameshika Mkataba wa Makubaliano ya usambazaji wa vifaa vya michezo ya Timu ya KMC FC.

Jeshi la Polisi linamshikilia mbakaji aliyetumia mtindo wa teleza
TAFIRI yatakiwa kufanya tafiti zenye tija kwa wavuvi wadogo