Kikosi cha KMC FC kinaendelea kujifua kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Young Africans ukataopigwa siku ya Jumamosi ya Aprili 10 katika uwanja wa Mkapa saa moja kamili jioni (19:00).

Katika mchezo huo KMC FC itakutana na Young Africans kwa mara ya pili huku ikiwa ugenini  kwenye msimu huu wa Ligi Kuu 2020/2021 umejipanga kuhakikisha kwamba inaleta furaha kwa mashabiki na kwamba wajitokeze uwanjani kutoa sapoti kwa wachezaji kwani Kino Boys inakwenda kupambania alama tatu muhimu kwenye mchezo huo.

KMC FC inatafuta ushindi huo ili kujiimarisha katika msimamo wa ligi Kuu na kwamba licha ya kuwa na upinzani mkubwa wakupambania alama tatu lakini bado mchezo huo upo ndani ya Timu ya Manispaa ya Kinondoni na kwamba hakuna kitakachoshindikana.

“Tunakwenda kwenye mchezo ambao kimsingi hautakuwa mwepesi kutokana na aina ya timu ambayo tunakutana nayo, ni nzuri, wanafanya vizuri, lakini pia wanaongoza ligi, hivyo mchezo utakuwa mgumu lakini pamoja na yote bado KMC FC tunasema kwamba tunakwenda kupambanania alama tatu na tunaimani kubwa yakufanya vizuri kwenye mchezo wetu.

Katika msimuu huu KMC FC ilikutana na Young Africans Oktoba 2020 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na kupoteza mchezo huo ambapo walifunga magoli mawili kwa moja, Goli la KMC lilifungwa na Hassan Kabunda kipindi cha kwanza katika dakika ya 23.

Imetolewa na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mahusiano wa Timu ya KMC FC

Rais wa Afrika Kusini amteua Mo Dewji kuishauri serikali ya nchi hiyo
Waziri kumaliza tofauti TFF, Young Africans