Vinara wa Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara KMC FC wamesisitiza kuwa na mipango madhuhuti ya kuendelea kuilinda nafasi hiyo, kwa kuhakikisha wanashinda kila mchezo ulio mbele yao.

KMC FC imeshinda michezo yote mitatu tangu kuanza kwa msimu huu 2020/21, na ipo kileleni ikifuatiwa Azam FC lakini tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa inazitofautisha timu hizo.

Kaimu Kocha Mkuu wa KMC FC, Habibu Kondo, amesema mikakati yake ni kuendelea kupambana hadi mwisho kutafuta alama muhimu katika kile mchezo ulio mbele yao dhidi ya Kagera Sugar.

Amesema kikosi chake kipo ‘fiti’ na baada ya kuibuka na alama tatu dhidi ya Mwandui FC, sasa wanaelekea mjini Bukoba kutafuta alama nyingine dhidi ya Kagera Sugar itakayochezwa kesho Ijumaa, Septemba 25.

“Msimu huu ligi ina ushindani mkubwa, nimejipanga kutafuta alama muhimu katika mechi zangu zote iwe nyumbani au ugenini ili kuhakikisha tunapata matokeo chanya na kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo,” amesema Kondo.

KMC ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya 13 ikiwa na alama 46, pointi moja zaidi ya timu zilizocheza mechi ya mchujo kuwania kujinusuru kushuka daraja, imeanza vema msimu huu huku pia ikiwa timu inayoongoza kwa kucheka na nyavu hadi sasa baada ya kufunga mabao manane na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara mbili tu.

Michezo mingine ya Ligi Kuu mzunguuko wanne itakayochezwa mwishoni mwa juma hili.

Suarez achomoka kilaini, Barca wakubali
Lowassa alivyomtumia ujumbe JPM, ‘inatisha lakini usitishike’