Mchezaji mkongwe wa timu ya mpira wa kikapu ya Los Angeles Lakers Kobe Bryant ametangaza kustaafu mchezo huo ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

Kobe , ambaye alisaidia Lakers kushinda mataji matano ya NBA baada ya kuwa katika NBA kwa zaidi ya miaka 20 ambayo yote ameichezea timu hiyo ya Los Angeles Lakers.

Kobe alitangaza Jumapili kwenye tovuti ya Wachezaji kwamba ameamua kustaafu baada ya msimu huu , huku akiandika kwamba msimu huu ndio pekee uliobakia kwake wa kuwapa alichonacho.

Kobe aliandika kwa mtindo wa shairi huku akiliita “Dear Basketball” na ndani yake kukiwa na maneno kadhaa ya kugusa moyo wa kila mpenda michezo.

Kobe Bryant ameshinda kila kitu katika NBA. Akicheza kwa miongo miwili yaani miaka 20, ameshinda tuzo ya MVP, kashinda medali za dhahabu za Olympic, kashiriki NBA All Star mara 17, ameshinda ubingwa wa NBA mara sita, kashinda tuzo za MVP za All star.

Pia ni mchezaji wa tatu aliyefunga pointi nyingi zaidi katika NBA

Kinachoendelea Ethiopia Chawakuna Azam FC
Wenger Aweka Pamba Masikioni Mwake