Kocha Mkuu wa Al Merrikh, Osama Nabieh amechimba mkwara mzito kuwa licha ya ubora wa kikosi cha Young Africans, wamejipanga kupindua meza na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Msafara wa kikosi cha AI Merrikh ulitua jijini Dar es salaam juzi Jumatano (Septemba 27), tayari kwa mchezo huo utakapigwa kesho Jumamosi (Septemba 30) katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini humo.

Nabieh ana kazi kubwa ya kuiongoza Al Merrikh kusaka ushindi wa mabao 3-0 ili kufuzu hatua ya makundi, hii ni baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Rwanda.

Akizungumza jijini Dar es salaam Kocha Osama amesema: Ni kweli tulicheza na timu bora, nadhani tulikuwa na mchezo bora sana Rwanda licha ya makosa kadhaa ambayo yalipelekea tukaruhusu kufungwa mabao mawili.

Zilikuwa dakika 45 za kwanza tumekuja Tanzania kwa ajili ya dakika 45 za kipindi cha pili, funafahamu utakuwa mchezo mgumu dhidi ya timu bora lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kufuzu hatua ya makundi tutapambana iwe jua, iwe mvua.

Dkt. Biteko aipatia Shule ya Sekondari Rusumo B Kompyuta 10
Janga lingine Chelsea, Pochetino athibitisha