Klabu ya Azam tayari ipo nchini Tunisia katika jiji la Sousse ilipoweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao, lakini kubwa zaidi ni uwepo wa kiungo Tape Edinho aliyekuwa kwa mkopo Stella Abidjan ya Ivory Coast.

Tape alitua Azam FC msimu uliopita na kusaini miaka mitatu, lakini katika dilisha dogo alitolewa kwa mkopo kwenda Abidjan ili kupisha usajili Mlinda Lango Abdulai Iddrisu na sasa Kocha Mpya, Youssouph Dabo amemrejesha.

Dabo aliuambia uongozi wa Azam FC kuwa anataka kuwaona wachezaji wote hata wale waliopo kwa mkopo, ndipo akina Edinho wakaitwa na katika mazoezi ya siku tatu yaliyofanyika Azam Complex kabla ya timu kusafiri, Dabo aliridhishwa na ubora wa Edinho.

Kocha huyo raia wa Senegal, Dabo amesema Edinho ni moja ya wachezaji wazuri na anaendelea kumjenga kuungana vyema na wenzake akiamini atakuwa bora zaidi msimu ujao.

“Nilichogundua wachezaji wote nilionao wana vipaji vikubwa akiwemo Edinho, hivyo tunachokifanya sasa ni kuwajenga wawe na muunganiko wa timu na kucheza kwa umoja jambo ambalo tunaamini litatusaidia,” amesema Dabo.

Ikumbukwe Azam FC msimu huu imefanya usajili wa wachezaji wanne, viungo Djibril Sylla (Gambia) na Feisal Salum Fei Toto’, mshambuliaji Alassane Diao na beki Cheikh Sidibe wote kutoka Senegal.

Thiago Silva: Nimemshawishi Paulo Dybala
Zinedine Zidane kurudi Santiago Bernabeu