Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Francic Baraza amemuonya Kiungo Mshambuliaji wa Young Africans, Denis Nkane kutoridhika na mafanikio aliyoyapata tangu ajiunge na kikosi hicho cha Jangwani kupitia dirisha dogo.
Baraza ametoa onyo hilo kwa Nkane kama KAKA ama MLEZI ambaye anatamani kuona akifika mbali zaidi, katika soka la ushindani na kuondoa mawazo ya kuamini Young Africans ndio mwisho wa safari yake.
Baraza aliyewahi kuwa Kocha wa Nkane akiwa Mkuu wa Benchi Ufundi la Biashara United Mara kabla ya kutimkia Kagera Sugar, amesema anamfahamu vizuri Mchezaji huyo kwa sababu alitambua uwezo wake na kumtambulisha katika Soka la Bongo msimu wa 2019/2020.
“Ninamfahamu vizuri sana Nkane, kwa sababu niliujua uwezo wake kisoka, nakumbuka ilikua msimu wa 2019-2020, nilipomka nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza katika Ligi ya Tanzania Bara.”
“Ni kijana mdogo mwenye kipaji kikubwa anayeweza kucheza sehemu yeyote,” amesema Baraza na kuongeza
“Young Africans ni timu kubwa na ina utofauti wa maisha na timu nyingine za ligi, namshauri Nkane asihisi amefika, bali alifanye lile kama daraja la kumfikisha mbali zaidi.”
“Hapaswi kujisikia wala kukata tamaa kwani bado mdogo sana, na safari yake kama ataendeleza nidhamu aliyonayo atafika mbali zaidi.” Amesisitiza Baraza
Tangu ajiunge na Young Africans kupitia dirisha dogo, Nkane amekuwa akipata nafasi ya kucheza lakini hajafunga bao lolote katika mShike MShike wa Ligi Kuu, tofauti na alipokuwa Biashara United Mara.